Korea Kaskazini imethibitisha kuwa rais Kim Jong-un ameongoza mwenyewe shughuli ya kufanyia majaribio makombora kadhaa ya masafa ya kadri na yale ya masafa ya mbali.
"Makombora kadhaa ya masafa mafupi pia" yalirushwa kutoka rasi ya Hodo hadi bahari ya Japan.
Kiongozi huyo alito igizo la kurushwa kwa makombora hayo ili "kuimarisha uwezo wa kujihami" kwa taifa, lilisema tangazo la shirika la kitaifa la habari la nchi hiyo.
Rais wa Marekani Donald Trump aliandika katika mtandao wake wa Twitter kuwa anaamini Bw. Kim hawezi kuvuruga uhusiano wao pamoja hatua waliyofikia katika harakati za kuleta usalama katika rasi ya Korea.
Aliongeza kuwa Kiongozi huyo wa Korea Kaskazini "anajua kuwa anaweza kunitegemea kwa hilina kwamba katu hatavunja ahadi yake kwangu. Muafaka utapatikan!
"Naamini kuwa Kim Jong-Un fana fahamu fika uwezo wa kiuchumi wa Korea Kaskazini na hatafanya lolote baya kurudisha kudidimiza matumaini hayo," Bw Trump aliandika katika Twitter yake
Kim Jong-un Aongoza Shughuli ya Kufanyia Majaraibio Makombora
0
May 06, 2019
Tags