Kocha wa Liverpool asema 'watapata tabu' kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya Barcelona

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema timu yake 'itataabika' leo usiku kwenye mchezo wa nusu fainali ya Klabu Bingwa Ulaya djhidi ya Barcelona.

Klopp pia amesema anaamini timu yake itapata nafasi katika mchezo huo utakaopigwa nyumbani kwa Barcelona, dimbani Nou Camp.

"Je, tutakuwa wakamilifu? Hilo haliwezekani. Tutafanya makosa? Hakika. Tutaabika, naam kwa asilimia 100," amesema kocha huyo raia wa Ujerumani.

"Kutakuwa na nyakati ambazo tutapata nafasi mchezoni? Kabisa, kwa asilimia 100. Natumai tutazitumia nafasi, na hicho ndicho tutajaribu kufanya."

Klopp, ambaye aliiongoza Liverpool mpaka fainali msimu uliopita pia amesema: "Tutakuwa huru kucheza mchezo wetu lakini wapinzani wetu ni timu nzuri sana."

Ajax yaingiza mguu moja katika fainali za vilabu bingwa Ulaya
Castor Semenya: Kwanini kesi yake ni muhimu
Tetesi za soka Ulaya Jumatano 01.05.2019
"Sisi tulikuwa kwenye mpambano mwaka jana, lakini wao wamekuwa kwenye mpambano kwa miaka karibu 20 sasa. Itakuwa mechi ngumu lakini naisubiri kwa hamu zote... Natumai wachezaji wangu nao wana ari kama yangu."

Kama ilivyo kwa Liverpool, Barcelona nao ni mabingwa mara tano wa kombe la Klabu Bingwa Ulaya.

Hata hivyo, Barcelona wameshinda makombe matatu ndani ya miaka 13 iliyopita. Wakati Liverpool imeshinda kombe lake la nne mwaka 1984 na la tano mwaka 2005.

Licha ya Liverpool kuwa na kikosi kikali chenye safu imara ya mashambulizi, Barcrlona hawajafungwa wakiwa nyumbani kwenye michuano hiyo kwa michezo 31 mfululizo sasa.

"Naweza sema tukipata sare hayatakuwa matokeo mabaya duniani, lakini si kama ndio tukitakacho, lakini itakuwa sawa tu," amesema Klopp ambaye pia aliiongoza Borussia Dortmund mpaka fainali ya michuano hiyo mwaka 2013.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad