Kocha wa Tottenham, Mauricio Pochettino azungumzia kikosi chake

Kikosi cha Tottenham hapo jana kimefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya Champions League kwa kuwafunga Ajax jumla ya mabao 3 – 2 kwenye mchezo huo huku usawa wa mabao ikiwa ni 3 – 3 na hivyo Spurs kufanikiwa kusonga mbele kutokana na mabao hayo ya ugenini.


Ushindi wa Spurs hautofautiani sana na ule wa Liverpool kwani hakukuwa na mtu yoyote aliyeamini kuwa timu hizi mbili kutoika nchini Uingereza zingeweza kutinga hatua hiyo ya fainali hasa kutokana na matokeo yao mabovu waliyopata kwenye michjezo yao ya kwanza ya Champions League.

Akizungumza kwa furaha mbele ya vyombo vya habari mara baada ya ushindi huo kocha Mkuu wa Tottenham, Mauricio Pochettino ameeleza hisia zake.

”Ni vigumu sana kufafanua hisia zangu zandani kupitia maneno, ila nafikiri ulikuwa usiku muhimu sana katika maisha yangu.” Amesema Pochettino

Mauricio Pochettino ameongeza ”Kwa namna mechi ilivyokwisha na kila kitu kilichotokea na vile tulivyopanga kucheza kwenye kipindi cha kwanza, nafikiri kilakitu kilikuwa chaajabu.”

”Kipindi cha pili tulipanga kufanya kidogo mabadiliko na kucheza kwa njia nyingine mbadala kilasiku naamini kutokata tamaa. Kuna mambo mengi sana kwenye kichwa changu ila nataka kuwapongeza sana wachezaji wangu kwakuumiliki mpira na kufanya kazi nzuri kwangu mimi nafikiri ni mashujaa, niliwaambia nafikiri miezi sita iliyopita narudia tena sentensi hii kuipeleka klabu fainali ya Champions League ni miujiza.”

Alipoulizwa kama kuna kitu chochote ambacho amejifunza kutoka kwa wachezaji wake kutokana na mechi hiyo na Ajax, Pochettino amesema ni kweli kipo.

”Nimejifunza mengi, kila kipindi unajifunza kutoka kwa wachezaji wako, wao ni walimu bora zaidi, wanaumiliki mpira na sio sisi makocha ninawashukuru sana na nina bahati kwakuwa nina kundi la wachezaji ambao kwangu ni mashujaa.”

Waandishi wa habari walipomuuliza Pochettino atawezaji kumfunga Liverpool kwenye mchezo huo wa fainali ya Champions League ambao umewakutanisha Waingereza watupu alisema.

”Naomba mniruhusu ni pumzike kiasi, nitahitaji muda wa kulizungumzia hilo kuhusu Liverpool. Nahitaji kumpongeza, Jurgen Klopp na wachezaji wake wote na Liverpool nafikiri walifanya maajabu.”

”Tulifurahi vya kutosha, kuanga namna gani walivyowashinda Barcelona, wao ni mashujaa pia na naamini itakuwa fainali ya maajabu sana kwa timu mbili za Uingereza na hakika tutakwenda kufurahia hilo.”

Hata hivyo kocha huyo wa Tottenham amezungumzia maisha yake ya baadae ndani ya timu hiyo mara baada ya kuulizwa na waandishi wa habari kama anampango wowote wa kuondoka kama atashinda taji hilo la Champions League ”Ndiyo nitaondoka nikishinda na pengine hata nikipoteza pia.” ameyasema maneno hayo huku akitabasamu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad