Kuomba Hela Ovyo Kulinigombanisha na Wazazi - Aunt Lulu

Kuomba Hela Ovyo Kulinigombanisha na Wazazi - Aunt Lulu
MTANGAZAJI Lulu Semagongo ‘Aunt LuLu’ ameibuka na kuifunua siri yake aliyokuwa ameificha muda mrefu kuwa, alikuwa kero kwa wazazi wake kutokana na tabia yake ya kuomba hela ovyo kwa watu.  Akipiga stori na safu hii, Aunt Lulu alisema alikuwa na tabia ya kuomba hela ovyo kiasi kwamba ilikuwa akikutana na wewe ukiona amekusalimia ujue kinachofuata ni kuomba shilingi kumi.

“Nilikuwa nikiomba shilingi kumi kwa kila niliyekuwa namsalimia, haijalishi barabarani au nyumbani, wewe ukiona nimekusalimia kinachofuata ni kukuomba hela, tabia hiyo ilinifanya nikagombana sana na wazazi wangu kwani walikuwa wanakerwa na mara nyingi walinikanya kwa kunichapa,” alisema Aunt Lulu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad