LHRC Kukusanya Taarifa za Ukiukwaji wa Haki za Binadamu Kidigitali

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, LHRC leo kimetambulisha rasmi na kuanza majaribio ya kutumia mfumo wa kidigitali katika ukusanyaji wa taarifa na matukio ya Ukiukwaji wa Haki za Binadamu.

Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Bi. Henga Anna amesema mfumo wa kidigitali wa ukusanyaji wa taarifa na matukio ya ukiukwaji wa Haki za Bindamu umezingatia mifumo yote ya kiusalama ili kumlinda mteja wao na kisheria hawaruhusiwi kutoa siri za mteja.

"Tumetengeneza mfumo wa kidigitali wa ukusanyaji wa taarifa na matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu ili tuweze kuwa karibu zaidi na watu ambao wako maeneo magumu huko vijijini na wanaomba tuwafikie kule waliko," amesema.

Ameendelea kwa kusema, "Kuna changamoto kubwa sana ya utoaji wa taarifa za ukiukwaji wa Haki za Binadamu, hii ni moja ya sababu ya kituo cha LHRC kuanzisha na kutumia mfumo wa kidigitali katika kukusanya taarifa za ukiukwaji wa Haki za Binadamu ili kuondoa changamozo hizo,".

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad