KLABU ya Lipuli imeiondoa Timu ya Yanga kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam baada ya kuipa kipigo cha bao 2-0, leo Jumatatu, Mei 6, 2019 kwenye Dimba Samora mjini Iringa.
Yanga wanatupwa nje, na Lipuli FC wanatinga fainali, sasa watakutana na Azam FC kwenye Dimba la Ilulu mkoani Lindi.