Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ameipa maagizo mazito Bodi mpya ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambapo ameipa miezi mitatu ya kufanyia maamuzi maagizo yake.
Waziri Lukuvi ametoa maagizo hayo katika Makao Makuu ya Wizara ya Ardhi jijini Dodoma wakati akizindua rasmi Bodi mpya ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambao wameteuliwa hivi karibuni .
Ameipa bodi hiyo mpya miezi mitatu ya kujifunza yale watakayoyasimamia kwani wengi wao wanatoka katika idara nyingine zisizo za NHC hivyo wapo huru kuchunguza idara yoyote na kama kuna mkurugenzi haoneshi ushirikiano wamlipoti na yeye atamchukulia hatua.
Mei 27 mwaka huu Uteuzi huu umefanyika baada ya kuvunjwa kwa Bodi hiyo Mwaka 2017 ambapo Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuri alimteuwa Mwenyekiti wa Bodi Dkt. Sophia Kongela kufuatiwa na baadae Mhe. Lukuvi kumteua Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba Maulid Banyani kukaimu nafasi hizo.
Wajumbe hao wapya ni pamoja na Bi. Sauda Msemo Kamishna Msaidizi Sera na Madeni Wizara ya Fedha na Mipango, Abdalla Mwinyimvua Mhasibu, Martin Madekwe Mstaafu kutoka Shirika la Nyumba la Taifa na Mr. Charles Singili Mkurugenzi Mtendaji Benki ya (TIB).
Wengine ni Immaculata Senje Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Makazi Wizara ya Ardhi, Ndg Humphrey Polepole Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mhandisi Mwita Rubirya ambapo kwa pamoja watashirikiana na Mwenyekiti wa bodi Dkt. Sophia Kongela pamoja na Mkurugenzi Mkuu Shirika la Nyumba Dkt. Maulid Banyani.
Maagizo Mazito ya Waziri Lukuvi kwa Bodi ya Wakurugenzi NHC
0
May 30, 2019
Tags