Maeneo Hatari Kwa Dengue Yatajwa DAR, Idadi ya Wagonjwa yapaa


Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Yudas  Ndungile amesema watu takribani 1,000 wameugua ugonjwa wa Dengue Jijini Dar es Salaam kuanzia mwezi Januari hadi mwezi Mei 2019 pia ametaja baadhi ya maeneo jijini Dar ambayo yana idadi kubwa ya maambukiz ya ugonjwa huo.

Ambapo ametaja maeneo hayo kuwa ni Ilala, Kariakoo, Upanga, Kisutu, Buguruni, Tabata, Mbezi, Ubungo, Kinondoni, Msasani na Masaki.

”Maeneo haya yamegundulika kuwa na wagonjwa wengine zaidi hivyo hatua zinapaswa kuchukuliwa ili kudhibiti maeneo hayo ikiwamo wananchi wenyewe kuchukua hatua” Ndungulile.

Dk. Ndungile amesema ugonjwa wa Dengue kasi yake ya kusambaa jijini Dar es Salaam imeongezeka, na kuwataka wakazi wa jiji hilo kuchukua tahadhari.

Aidha, amewataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kusafisha mazingira yanayowazunguka ili kuondoa mazalia ya mbu wanaoeneza ugonjwa wa Dengue.

Na ameshauri Wananchi kufika hospitalini na katika vituo vya afya mapema pindi wanapo ona mabadiliko ya afya zao, ili wafanyiwe uchunguzi wa kitabibu, huku akisisitiza kwamba ugonjwa huo unapimwa bure.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad