Makanisa ya Kilokole na Udanganyifu Mwingi Kwa Jamiii...Tufanye Kazi Ndugu zangu Hakuna Njia Rahisi
0
May 20, 2019
Makanisa mengi ya siku hizi ni kutoa mapepo , kuuza maji, kuuza mafuta c, kufanya miujiza fake , uponyaji fake , wachunguji wanalala na waumini , wizi, utapeli, ulaghai na kila aina ya false doctrine!
Wenye shida wanajikuta wanazamishwa kwenye dhiki kuu.
Soluhisho:
Ukiumwa nenda hospitali
Kama una shida na fedha fanyakazi badala ya kukesha sijui na maombi mikesha ya makelele ongeza bidii kazini !
Ukitaka kuolewa kuwa na tabia njema huwezi pata mchumba huku una kesha ukifanya Zinaa kanisani ukifikiri wachumba hawajui !
Badala ya kukesha unadanganywa na wachungaji fake soma biblia - kusali sio lazima mpaka uende utafute matapeli walipo sali huku unalima.
Muujiza wa kweli ni kufanya kazi kwa bidii.
Na wale waliopo kwenye ndoa kila anayefikiri eti kuna mchungaji anaweza kutatua matatizo ndani ya ndoa yako jua hiyo ndoa imevunjika. Fix problem hakuna sala ya tapeli inatatua Tatizo !
Acheni kuabudu majizi!
Mungu hana ushirika na mtu na hakuna wa kumpelekea habari ya mwingine Pambana na hali na ongea na Mungu mwenyewe atakusikia!
Hii kitendo mnachomfanyia dhihaka Mungu hawezi kuwaacha salama !
Kuanzia Leo kila atakayesoma haya azinduke ! Achaneni na mikusanyiko ya matapeli wanaoibia watu kwa kujifanya wahubiri, mnabii, wachungaji , maaskofu fake .
Ukiona mtu anatumia nguvu sana kutaka umkubali kama mtumishi wa Mungu huyo mwizi na tapeli !
Usinunue kitu chochote eti kina Baraka au muujiza . Neema za Mungu haziuzwi.
Mawe na ya sikie !
Na ukijua ina imani ya mwendo kasi acha kupoteza wengine !
Waliotabiriwa wameongezeka kwa kasi ya moto wa kifuu.
Tubuni na kuiamini injili .
Ukikutana na mtu anakuambia sijui pastor wangu , Nabii wangu sijui mchungaji wangu anafanya hivi au vile Kimbia hao ni na agent wa shetani !
Imeandikwa umepewa bure toa bure .
Siku za mwisho matapeli na wafuasi wa shetani ni wengi wanataka kuangamiza taifa la Mungu waepukeni .
Tags