MALAWI: Kiongozi wa Upinzani Lazarus Chakwera Achukua Uongozi wa Nchi Mapema


Kiongozi wa upinzani nchini Malawi amechukua uongozi wa mapema katika uchaguzi mkuu uliofanyika mnamo mwezi Mei 21, kulingana na tume ya uchaguzi nchini humo.

Lazarus Chakwera , kiongozi wa chama cha upinzani cha Malawi Congress Party MCP amejipatia kura 533,217 ambayo ni sawa na asilimia 37.65.

Anafuatiwa kwa karibu na rais wa sasa Peter Mutharika ambaye ana kura 524,247 ikiwa ni asilimia 37.1 huku makamu wa rais Saulos Chilima wa United Transformation Movement akiwa wa tatu na kura 293,978 ambayo ni asilimia 20.76.

Kiongozi wa chama cha zamani zaidi nchini Malawi Lazarus Chakwera amesema kuwa matokeo hayo ya mapema yanampatia uongozi katika uchaguzi huo.


Amesema kwamba kuna jaribio la baadhi ya watu wasiojulikana kuingilia matokeo ya uchaguzi huo yanayopeperushwa moja kwa moja katika kituo kikuu cha uchaguzi mjini Blantyre akiapa kwamba hatokubali uchakachuaji wwote.

Lakini tume ya uchaguzi nchini humo imetoa wito wa kuwepo kwa utulivu ikisisitiza kuwa ndio yenye uwezo wa kutangaza matokeo hayo.

Uchaguzi huo umekumbwa na ushindani wa karibu kati ya rais Peter Mutharika , makamu wake Saulos Chilima na Chakwera ambaye anakiongoza chama cha Malawi Congress party.

Katika uchaguzi wa 2014 , Chakwera alipoteza kwa karibu dhidi ya rais Mutharika na akashindwa kupinga uchaguzi huo mahakamani.

Tume ya uchaguzi ina hadi siku nane kutangaza matokeo hayo .

Hatahivyo imekiri kwamba inakabiliwa na changamoto za kiufundi katika utangazji wa matokeo hayo.

Hatahivyo inasema kuwa ina imani kwamba itatoa matokeo yalio huru na haki.

Takriban raia milioni 6.8 wa Malawi walisajiliwa kushiriki katika uchaguzi huo kumchagua rais mpya , mbunge mpya na madiwani.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad