Mapigano makali Yaibuka Tena Libya Kati Ya vikosi vya Haftar na vya serikali ya umoja wa kitaifa

Vyombo vya habari vya Libya vimetangaza kujiri mapigano makali jana usiku kati ya vikosi vya kundi linalojiita jeshi la kitafa la Libya linaloongozwa na Jenerali Khalifa Haftar na vile vya serikali ya umoja wa kitaifa ya nchi hiyo kusini mwa mji mkuu Tripoli.

Vyombo hivyo vimetangaza kuwa hadi jana usiku mapigano makali kati ya pande mbili hizo yalikuwa yakiendelea katika eneo la barabara inayoelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Tripoli na katika eneo la al Aziziyah yapata umbali wa kilomita 45 kusini mwa mji mkuu.

Mapigano katika mji mkuu wa Libya Tripoli yanaendelea  katika hali ambayo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juzi Ijumaa lilitaka kutekelezwa usitishaji mapigano nchini humo na pande zinazozozana kurejea kwenye meza ya mazungumzo.

Kundi linalojiiita jeshi la kitaifa la Libya chini ya kamanda Khalifa Haftar ambalo kwa miaka kadhaa limekuwa likidhibiti maeneo ya mashariki mwa Libya kutokana na uungaji mkono wa Saudi Araba, Misri, Imarati na baadhi ya nchi za magharibi katika miezi ya karibuni lilisonga mbele kuelekea upande wa kaskazini mwa nchi.

 Jenerali Haftar tarehe nne Aprili mwaka huu aliwaamuru wapiganaji wake kuanzisha mashambulizi ya pande zote dhidi ya mji mkuu Tripoli kwa kuungwa mkono na nchi hizo tajwa. 

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), zaidi ya watu 440 wameshauawa na zaidi ya 2000 wengine wamejeruhiwa tangu yalipoanza mashambulizi hayo, mbali na watu 55 elfu wengine kukimbia makazi yao kutokana na vita hivyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad