Meli hiyo kwa jina Wise Honest imedaiwa kutumia kusafirisha mkaa na mashine nzito.
Marekani imeikamata meli ya Korea Kaskazini ikiilaumu kwa kukiuka vikwazo vya kimataifa.
Idara ya haki imesema kuwa meli hiyo ilitumika kusafirisha makaa hayo ambayo ndio biashara kubwa ya taifa hilo licha ya kupigwa marufuku na Umoja wa mataifa kuendelea kuyauza nje
Meli hiyo ilikuwa imekamatwa nchini Indonesia mnamo mwezi Aprili 2018.
Ni mara ya kwanza Marekani imeikamata meli ya Korea Kaskazini kwa kukiuka vikwazo na hatua hiyo inajairi wakati ambapo uhusiano kati ya mataifa hayo mawili umedorora.
Mamia ya waombolezaji wamiminika kumuaga
Mkutano kati ya kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un na rais wa Marekani Donald Trump uliisha bila makubaliano mnamo mwezi Februari huku Marekani ikiisisitizia Korea Kaskazini kusitisha mpango wake wa kinyuklia huku nayo Pyongyang ikisisitiza kuondolewa vikwazo.
Korea Kaskazini imetekeleza majaribio mawili ya makombora yake angani katika kipindi cha wiki moja katika kile kinachoonekana kuwa jaribio la kuishinikiza Marekani kufanya makubaliano.
Je tunajua nini kuhusu meli hiyo?
Meli hiyo , kwa Jina the Wise Honest , ilikamatwa mara ya kwanza mwaka uliopita na Marekani ilitoa kibali cha kuikamata mnamo mwezi Julai 2018.
Indonesia imeikabidhi Marekani meli hiyo na sasa inaelekea Marekani.
Maafisa wa Marekani wamesema kuwa tangazo hilo halitokani na majaribio ya makombora yaliofanywa na Korea Kaskazini.
Afisi yetu iligundua mbinu ya Korea Kaskazini kuuza nje tani za makaa ya mawe ya kiwango cha juu kwa wanunuzi wa kigeni kwa kuficha asili ya meli , The Wise Honest , alisema mwendesha mashtaka wa Marekani Goeffrey S Berman.
Marekani yaikamata meli ya Korea Kaskazini kwa kukiuka vikwazo
0
May 10, 2019
Tags