Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili, Yusuf Ali Yusuf, maarufu kama ‘Mpemba wa Magufuli’ imeshindwa kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa sababu mashahidi wamekwenda kwenye Oparesheni maalum ya Jeshi la Polisi.
Yusuf na wenzake watano wanakabiliwa na mashtaka manne ikiwemo kujihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh.Milioni 785.6.
Wakili wa Serikali Elizabeth Mkude, ameeleza kuwa Mei 30, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kusikilizwa lakini mashahidi wako nje ya mkoa na mwingine waliyemtegemea ni mgonjwa.
Baada ya maelezo hayo Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Juni 13 na 19, 2019 kesi hiyo itakapotajwa na washtakiwa wamerudishwa rumande kutokana na mashtaka yanayowakabili kutokuwa na dhamana.
Mbali na Yusuph(35), washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Charles Mrutu(37), maarufu kama mangi mapikipiki na mkazi wa Mlimba, Morogoro; Benedict Kungwa(40), mkazi wa Mbagala Chamazi; Jumanne Chima(30), maarufu kama JK na mkazi wa Mbezi; Ahmed Nyagongo(33), dereva na mkazi wa Vikindu-Mkuranga na Pius Kulagwa(46)mfanyabiashara na mkazi wa Temeke.
Miongoni mwa shtaka moja kati ya mashtaka manne yanayowakabili wanadaiwa kati ya Januari, 2014 na Oktoba, 2016, katika maeneo ya Jiji la Dar es Salaam, Tanga, Iringa na Mtwara, walijihusisha na mtandao wa ujangili kwa kukusanya na kuuza nyara za Serikali ambazo ni vipande 50 vya meno ya tembo vyenye thamani ya dola za Marekani 180,000 sawa na Sh. 392,817,600 bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori
Mashahidi Wakwamisha Kesi ya ‘Mpemba wa Magufuli’ Mahakamani Imepanga Haya
0
May 31, 2019
Tags