LMkazi wa kijiji cha Nduku wilayani Kahama mkoani Shinyanga SAMORA MASABI amefikishwa katika Mahakama ya wilaya ya Kahama kwa Tuhuma ya kumbaka na kumpa mimba mwanafunzi mwenye umri wa miaka 16.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo EVODIA KYARUZI Mwendesha Mashitaka wa Jeshi la Polisi SHABANI MATESO amedai SAMORA aliteda kosa hilo kati ya Disemba 12 mwaka jana na Januari mwaka huu katika kijiji hicho.
Amesema Mtuhumiwa baada ya kutenda Makosa hayo alitoroka kusiko julikana hadi alipokamatwa na Jeshi la Polisi Mei 20 mwaka huu na kufikishwa mahakamani leo kujibu Tuhuma zinazo mkabili.
Katika Shauri hilo la Jinai namba 190 la mwaka huu MATESO amesema SAMORA anashitakiwa kwa Makosa mawili ambapo kosa la kwanza ni la kumbaka Mwanafunzi kinyume na kifungu 130(1)(2) na 131 sura 16 ya sheria ya makosa ya jinai marejeo ya mwaka 2002.
Katika shitaka la pili SAMORA anatuhumiwa kumpa mimba mwanafunzi huyo kinyume na fungu la 60(A) sura 353 ya sheria ya elimu namba 2 ya mwaka 2016.
SAMORA amekana mashitaka yote yanayomkabili na Shauri hilo limeahirishwa hadi June 10 mwaka huu litakapotajwa tena Mahakamani na amerudishwa Rumande kwa kukosa dhamana.