Mbinu Rahisi za Kupata Ujasiri wa Kimafanikio


Chanzo kikuu cha mafanikio ni pamoja na mtu husika kuwa jasiri, ujasiri wa kutaka kweli kufanikiwa na si vinginevyo. Zifutazo ndizo mbinu rahisi za kuapata ujasiri wa mafanikio;

1. Kutoshindana na waliofanikiwa.
Daima mtu ahakikishe anawafanya waliofanikiwa wajione wapo juu. Kama mtu anataka kuwashangaza basi asionyeshe ujuzi wake wote. Kuwapa waliofanikiwa heshima yao kutamfanya mtu apate msaada na hatimaye afikie kiwango cha juu bila ya kupata tabu nyingi.

Mfano, mtu asishindane na mwajiri wake ili kuonekana anajua sana; asishindane na tajiri katika matumizi hususani mazingira ya kijamii kama baa, misiba n.k. Waliofanikiwa hutafsiri kitendo cha kushindana kama kuonyesha kiburi au maskini jeuri.

2. Kutoamini sana marafiki.
Mtu awe makini 'anapojamiiana' na marafiki au watu wa karibu. Watu wa karibu huwa wasaliti na huvujisha siri kwa wapinzani. Mtu aogope marafiki zaidi ya maadui, ikibidi awape nafasi wale anaohisi ni wapinzani. Ilikiwa mtu hana wapinzani, ajitahidi kuwatafuta. Mtu ajifunze jinsi ya kutumia wapinzani kimafanikio, si kuwaamini marafiki muda wote.

3. Kuficha malengo.
Mtu afiche matarajio yake au dhamira za matendo yake. Kuweka malengo hadharani huwafanya watu wenye nia mbaya kujipanga na kuvuruga malengo husika. Mtu akinge malengo yake na ikiwa yatagundulika iwe nyakati za mwisho; nyakati ambazo wapinzani hawawezi kuweka vikwazo.

4. Kutumia wasidizi.
Kufankiwa kwa mtu kunategemea mchango anaoupata kutoka kwa wale wanaomzunguka (mazingira na marafiki). Mtu atumie busara, ujuzi na maarifa ya wale anaofanya nao kazi ili kusonga mbele. Msaada haupunguzi tu nguvu, bali pia huongeza ufanisi na kuimarisha urafiki. Mtu hupata fadhila kutoka kwa wasaidizi wake, ndipo jamii husika. Hivyo, mtu awaachie watu wengine yale wanayoweza kufanya kwa ufanisi.

5. Kushinda kupitia matendo.
Ushindi mtu anaopata kupitia maneno haufai kitu! Mtu asishindane juu ya uwezo wake kwa maneno bali, aache matendo yaongee. Ushindi makini ni ule mtu anaoupata kupitia matendo yake, na si kwa wingi wa maneno. Uhalisia wa matendo huonyesha umakini wa mtu kwa jamii inayomzunguika. Mtu husifiwa kwa kadiri ya juhudi zake za hali na mali kutatua changamoto zinazomsonga, si kwa kupiga domo.

6. Kujenga utegemezi.
Ili mtu kujua umuhimu wake katika jamii anapswa kujua kwa kiasi gani mchango wake unahitajika. Mtu ajenge mazingira ya kutegemewa; kutegemewa kuleta furaha au ustawi katika mazingira yanayomzunguka.

Ili kufanya hivyo, mtu asitoe mbinu zote alizo nazo juu ya kitu fulani. Kutegemewa humwezesha mtu 'kuuza' kile alichonacho kwa mafanikio yake na ya jamii yake. Hivyo, mtu ajue wakati gani wa kuficha huduma yake, wakati gani wa kutoa kidogo na wakati gani wa kutaka watu wailipie.

7. kutenda kama mpelelezi.
Ni muhimu sana mtu kujua juu ya wapinzani wake. Mtu atumie marafiki (wapambe) ili kupata taarifa muhimu juu ya udhaifu na uwezo wa wapinzani wake. Kufanya hivyo kutamwezesha mtu kupanga mipango ya kiulinzi na ambayo haitazimika katika safari yake ya mafanikio. Kupata taarifa kunafanikishwa kwa kuuliza maswali rahisi, kuuliza kwa njia ya upole na kwa kutumia mifano. Kila wakati ni fasaha kwa upelelezi.

8. Kuwafahamu watu wa karibu.
katika mazingira yoyote yale kuna watu wa aina nyingi. Watu hutofautiana kiimani, kitabia, kimalengo, kiutendaji n.k. Watu wa karibu ndio wanaotoa au kufanikisha kotoa ushindani katika mazingira yasiyotegemewa. Watu wengi, tena wa karibu ni kama mbwa mwitu. Ili kufahamu watu wa karibu, mtu atafakari kwa kina misingi mikuu ya urafiki huku akibadilisha muonekano, kutoa changamoto kwa walengwa n.k. Pindi mtu anapofanya yote hayo atazame mwitikio ya walengwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad