Mbowe Amchana Hadharani Kiongozi Aliyetoa Maneno ya Kibaguzi

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Mbowe amesema kuna jambo ambalo hajalipenda, jambo ambalo limesemwa kuwa watu wa Kabila fulani hawawezi kutoa misaada kwa Walemavu.

Mbowe ameyasema hayo leo, alipokuwa akitoa salamu za rambirambi katika ibada ya kumuaga aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni tanzu za IPP, Dk. Reginald Mengi iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro.

“Kuna kauli zinasemwa sana watu na kwa ukweli zinakera kwa vile mimi si mnafiki lazima niseme na nitasema hapa hapa mbele za watu.

“Tuna nchi moja ambayo tunastahili kupendana na kusaidiana, na kila mtu ana haki ya kumsaidia mwenzie, tusikubali kauli za viongozi zitugawe na hasa za kidini na kikabila, kauli ya kusema kuna makabila hayawezi kuwasaidia walemavu si nzuri na haikutupendeza kwa kweli, tujitafakari tunapotaka kuongea maneno,” amesema Mbowe.

Mbowe alisema maneno hayo pasipo kumtaja kiongozi nani aliyesema maneno hayo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad