Amesema hayo leo Jumatatu Mei 20, 2019 bungeni jijini Dodoma katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Kilimo mwaka 2019/2020.
Amesema nchi nne barani Afrika zimeruhusu kilimo cha bangi kwa ajili ya matumizi ya dawa za binadamu.
“Amebainisha dawa nyingi za maumivu ya saratani asilimia 80 zinatokana na bangi, “Nashangaa wataalam wetu wa Mamlaka ya Chakula la Dawa (TFDA) wangekuwa wameshachukua sampuli na wangewajulisha kuwa dawa zilizo na bangi ndani yake.”
“Wangemuuliza msambazaji hiyo bangi anaitoa wapi? Spika sisi wenyewe tunayo bangi hiyo tunaona kila siku inakatwa ukweli nyingi sio kwa ajili ya kuvuta. Bangi hiyo imekuwa ikienda katika dawa za binadamu.”
Amesema ana ushahidi Lesotho na Zimbabwe kuruhusu ulimaji wa bangi na kuna viwanda vya kutengeneza dawa za binadamu kwa kutumia bangi.
Amesema gunia moja la bangi nchini ni kati ya Sh4milioni hadi Sh4.5milioni na kwamba Lesotho na Zimbabwe gunia moja ni Sh20milioni.
“Bangi yote ya Tanzania inakwenda katika dawa za binadamu ambazo tunaletewa kutumia. Kuna ubaya gani ikaanza kutoa vibali kwenye maeneo mbalimbali na kuhalalisha watu waanze kulima bangi hiyo na kupata faida.” amesema.
Amesema haungi mkono kauli ya mbunge wa Geita (CCM), Joseph Msukuma ambaye amekuwa akitaka bangi kuhalalishwa kwa ajili ya kuvuta.
Akichombeza Spika Ndugai aliwataka Wabunge kuchangia kama ambavyo amechangia Mbunge huyo kwa kujikita katika eneo moja
“Niwape siri muongee kama Kishimba unakuja na kitu chako fulani.unajikita sehemu moja.Hii hoja ni nzuri sana Naamini Jenista (Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge,Ajira,Kazi,na watu wenye ulemavu) ameipigia mstari,”amesema Spika Ndugai.