Mbunge wa Nsimbo Atishia Kuvua Nguo Bungeni Kisa Maji

Mbunge wa Nsimbo atishia kuvua nguo bungeni kisa maji
Mbunge wa Nsimbo, Richard Mbogo (CCM), ametishia kuvua nguo bungeni ikibidi ili yapatikane maji safi na salama kwenye jimbo lake.

Mbogo ametishia hivyo wakati akichangia mjadala wa Wizara ya Maji bungeni leo Mei 3, ambapo amesema suala la maji halina mbadala hivyo Serikali itatue tatizo hilo jimboni mwake.

Amesema kama ilivyokuwa kwa mtumishi wa Mungu, Ibrahimu, alikuwa tayari kumchinja mwanawe, lakini baadaye Mungu alimpatia mwanakondoo wa kuchinja, mwanawe akanusurika.

“Mheshimiwa mwenyekiti, suala la maji safi na salama si la mzaha, ikibidi niko tayari kuvua nguo hapa bungeni ili nipate suluhisho la upatikanaji wa maji Nsimbo.

“Kama kuonyesha niko ‘serious’ kwa jambo hili niko tayari kufanya lolote, kama kuna jambo mnaweza kufanya mtuambie tufanye, tozo hii ya Sh. 50 ni muhimu sana,” amesema Mbogo
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad