Mbwana Samatta Aonyesha Udume Wake..Atwaa tuzo ya 'Kiatu cha Ebony' Ligi ya Ubelgiji



Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta ‘Samagoal’ anayechezea KRC Genk ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora Mwafrika katika Ligi ya Ubelgiji, ijulikanayo kama Jupiler Pro League.

Samatta ameshinda tuzo hiyo iitwayo ‘Kiatu cha Ebony katika sherehe za tuzo za Jupiler Pro League usiku wa Jumatatu mjini ukumbi wa Birmingham Palace mjini Brussels.

Samatta anakuwa mchezaji wa tatu tu wa Genk kushinda tuzo hiyo baadfa ya Oulare mwaka 1999 na Dagano mwaka 2002.

Pamoja na Samatta, Genk pia imetoa kocha Bora wa Msimu wa Jupiler Pro League, ambaye ni Kocha wake Mkuu, Mbelgiji Philippe Clement.

Nyota wengine wa KRC Genk walioingia kwenye kinyanganyiro lakini wakatoka kapa ni Malinovskyi na Pozuelo (Mchezaji Bora) na Promise (Sander Berge).

Ikumbukwe Samatta ameshinda tuzo hiyo baada ya kazi nzuri msimu huu, akiisaidia Genk kukaribia kutwaa ubingwa wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad