Misingi ya Kuifahamu Katika Kujenga Nidhamu ya Pesa



Ili tuweze kufikia malengo tuliyojiwekea katika maisha yetu hatuna budi kuwa na nidhamu ya fedha inayotokana na kipato chetu cha kila siku.

Kuwa na nidhamu ya kifedha ndiko kutakotusaidia kuweza kuishi maisha yenye tija katika ulimwengu huu hii ni kwa sababu tutakuwa tunaheshimu kila pesa tuyoipata na kila pesa tunayoitumia.

Nidhamu ya fedha  ni lazima iwe kati ya haya yafuatayo;

Kila wakati jifunze kuweka akiba kutokana na kipato chochote ulichonacho au unachokipata. Mfano unaweza kuwa unjiwekea hata kuanzia kianzio kidogo sana katika benki, huduma za kifedha kupitia simu.

Kiasi chaweza kuanzia 1000, 5000,10000  kiasi hicho kitatokana na maamuzi yako wewe mwenyewe kutokana na vile unavyopata.

Epuka matumizi yasiyo rasmi au lazima. Fanya matumizi kwa vitu unavyovihitaji na wala siyo vile unavyovitaka.

Mfano tumia fedha kulipa ada, kodi,mavazi ya lazima, kununua chakula, bili za maji au umeme na vitu vingine vilivyo muhimu binadamu kuwa navyo au vile vinavyompasa binadamu kutumia pesa. Usitumie pesa kulewa hovyo,kutafuta sifa kwa kuagiza round nyingi kwa ajili ya washikaji, kuonga au kugawa pesa hovyo bila sababu maalumu.

Iwekeze pesa yako ili ikue na kuzaa zaidi. mfano fungua biadhara au miradi itakayozalisha pesa yako mara dufu zaidi.

Weka malengo hai ya maisha yako ambayo yataongoza katika matumizi sahihi ya fedha yako.

Epuka mikopo mibaya. Mfano kukopa ili  ununue usafiri,uchangie harusi, kununua gari la starehe n.k. bali unaweza kukopa kununua kiwanja au kujenga nyumba za kibiashara maana vitu hivyo thamani yake huongezeka kila leo.

Kuwa na akiba ya dharula kama magonjwa, ajali au msiba.
 Hivyo wito wangu kwako  leo ni  ujifunze kutumia fedha yako kwa usahihi zaidi ili baadae usije kujuta.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad