Mkapa Nae Afunguka Makubwa Kuhusu Mengi aeleza alivyosaidiwa



Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Dkt. Benjamin Mkapa ameeleza masikitiko yake kufuatia msiba wa aliyekuwa Mwenyekiti wa makampuni ya IPP, Dr. Reginald Mengi kilichotokea Mei 2, huko Dubai.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi yake, Mkapa ameeleza mchango wa Dr. Mengi katika maendeleo ya taifa wakati wa uongozi wake.

“Wakati wa urais wangu, Dr. Mengi kupitia shughuli mbalimbali alinifanya niwe Rais mzuri. Alikuwa mkweli katika maoni yake hata kama yalikuwa tofauti na misimamo yangu lakini hilo lilinifanya kufaidika na busara zake,” alisema Rais huyo mstaafu.

Aidha Mkapa aliyeongoza nchi kuanzia mwaka 1995 hadi 2005, ameongeza kuwa, utumishi wa Mengi katika sekta binafsi umeendelea kuwa muhimu hadi leo na anatambulika kama mtu aliyemshawishi kila anayetamani kuona nchi ikiendelea.

Alisema namna pekee ya kumuenzi ni kufuata njia na mifano aliyoionyesha, kwamba kupambana na umasikini siyo jukumu la Serikali peke yake bali ni la kila mtu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad