Moto wa Sekondari ya Ashira Wazua Utata, Iweje Mabweni Mawili Yaliyotengana Yaungue Kwa Pamoja



Moshi. Moto ambao chanzo chake bado hakijajulikana, umeteketeza mabweni mawili ya ghorofa ya shule kongwe ya Sekondari ya Wasichana ya Ashira, huku kiini cha moto huo kikiacha maswali mengi.

Utata unaojitokeza ni jinsi majengo mawili yasiyotegemeana kwa umeme kuungua kwa wakati mmoja.

Tukio hilo ambalo limesababisha uharibifu mkubwa wa vifaa vya wanafunzi na vingine vilivyokuwa kwenye mabweni hayo, lilitokea jana asubuhi wakati wanafunzi wakiwa madarasani.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira akizungumzia tukio hilo alisema,
“Hivi tunavyozungumza, vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na kikosi cha Zimamoto na Uokoaji wako eneo la tukio na tathmini ya madhara itatolewa baada ya uchunguzi.”

Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba aliliambia Mwananchi kuwa wanafunzi 73 wamepoteza vifaa vyao vyote ambavyo ni pamoja na mavazi.

Alisema kwa taarifa za awali, tukio hilo linaonyesha halijasababishwa na hitilafu ya umeme na kwamba uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo chake

By Waandishi Wetu, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad