Rais wa Malawi Peter Mutharika amethibitishwa na tume ya uchaguzi kunyakua muhula wa pili madarakani baada ya kupata ushindi mwembamba wa asilimia 38.7 ya kura.
Mwenyekiti wa chama cha upinzani cha Malawi Congress Party Lazarus Chakwera, ameibuka nafasi ya pili na asilimia 35.41 ya kura wakati makamu wa rais Saulos Chilima akipata asilimia 20.24.
Uchaguzi wa rais na wa bunge ulifanyika Jumanne iliyopita, ambapo matokeo yalitarajiwa kutolewa mwishoni mwa Juma.
Hata hivyo tume ya uchaguzi ya Malawi ilisitisha kutangaza matokeo ya mwisho siku ya Ijumaa baada ya mahakama kuu kuamuru hivyo kutokana na malalamiko 147 yaliyowasilishwa ya hitilafu katika uchaguzi ikiwemo karatasi za kupigia kura zilizokuwa zimefutwa kwa kutumia wino wa kufanya masahahisho.
Baadae Jumatatu mahakama iliondoa amri hiyo na tume ya uchaguzi kuthibitisha ushindi mwembamba wa Mutharika.
Mutharika athibitishwa na tume kushinda muhula wa pili Malawi
0
May 28, 2019
Tags