Mwanaharakati maarufu wa kupigania haki za wapenzi wa jinsia moja Kenya amefariki

Mwanaharakati wa kupigania haki za wapenzi wa jinsia moja nchini Kenya Binyavanga Wainaina amefariki. Nduguye James Wainaina amethibitisha kwa BBC

Mwanaharakati huyo amefariki akiwa na umri wa miaka 48.

Wainaina alikuwa mshindi wa tuzo ya Caine na aliorodheshwa na gazeti la Times magazine miongoni mwa watu 100 wenye ushawishi mkubwa duniani 2014.

Ni miongoni mwa Wakenya wa kwanza kutangaza hadharani kwamba ni mpenzi wa jinsia moja.

Amefariki siku mbili tu kabla ya mahakama nchini Kenya kutoa uamuzi wa iwapo itafutilia mbali sheria za kikoloni ambazo zinaharamisha haki za wapenzi wa jinsia moja.

Binyavanga Wainaina, aalikuwa miongoni mwa wakenya wa kwanza kujitokeza hadharani na kusema kuwa yeye hushiriki mapenzi ya jinsia moja.

Tangazo hilo lilimfanya Binyavanga kuwa mmoja wa waafrika mashuhuri kujitokeza hadharani.

Alifichua hali hii katika taarifa yake kupitia kwa mtandano wa kijamii wa Twitter iliowiana na siku ya kuzaliwa kwake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad