Siku mbili baada ya mwili wa bilionea wa Tanzania marehemu Reginald Abraham Mengi kuwasili mjini Dar es Salaam mwili wa mwanzilishi huyo wa makampuni ya IPP umewasili mjini Kilimanjaro tayari kwa mazishi yake.
Mamia ya marafiki na watu wa familia walikongamana katika uwanja a ndege wa Kilimajaro kuupokea mwili wa mfanyibiashara huyo na msomi aliyefariki akiwa na umri wa miaka 75.
Kulingana na mtandao wa The Citizen nchini Tanzania Baadaye msafara wake unatarajiwa kuelekea nyumba kwa marehemu katika eneo la machame wilaya ya hai ambapo waombolezaji watamuombea.
Kulingana na vyanzo vya familia mwili huo unatarajiwa kupelekwa hadi Moshi mjini mapema Alhamisi alfajiri ambapo wakaazi wa eneo hilo watatoa heshima zao za mwisho kwa mtu aliyekuwa maarufu kwa kuwasaidia wengi.
Kamanda wa jimbo la Kilimajaro Anna Mwira alisema kuwa hatua ya kuusafirisha mwili huo hadi Moshi ilitokana na ombi la watu wengi ili kuwqaruhusu watu wa Moshi kutoa heshima zao za mwisho.
Tulikuwa tumejiandaa kufanya kila kitu katika eneo la Machame lakini kukatokea ombi kutoka kwa wakaazi waliofanya kazi kwa karibu na kumjua marehemu kutoa heshima yao ya mwisho, alisema kamishan huyo wa eneo la Kilimajaro.
Mazishi yake kulingana na msemaji wa familia Michael Ngalo yatafanyika hapo kesho baada ya misa ya wafu.
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, ameongoza mamilioni ya Watanzania kutuma salamu za rambirambi kufuatia msiba huo.
Kupitia ukurasa wake rasmi wa mtandao wa kijamii wa Twitter Magufuli amesema ataendelea kumkumbuka Mzee Mengi kwa mchango wake katika maendeleo ya taifa lake