Mwili wa Dkt. Mengi Waagwa Karimjee

MWILI wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi,  umewasili  katika Ukumbi wa Karimjee, ulioko Posta jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutolewa heshima za mwisho na kuagwa leo Jumanne, Mei 7, 2019.

Familia ya marehemu Dkt. Reginald Mengi wakiwemo watoto na mjane wake, Jacqueline Mengi (mwenye miwani) wakiwasili katika ukumbi wa Karimjee.

Viongozi mbalimbali akiwemo Rais John  Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu, viongozi mbalimbali wa serikali, vyama vya siasa, taasisi, dini na wananchi wamejitokeza kwa ajili ya kutoa heshima zao za mwisho kwa Mengi.


Nje ya Ukumbi  kuna wanafamilia wengi wa Mengi ambao si ndugu zake wa damu, wengine hawajawahi hata kuonana naye lakini aligusa maisha yao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad