Nape Afanguka Alivyopewa Pesa na Dkt. Mengi Kwenye Begi


MBUNGE wa Mtama (CCM), Nape  Nnauye,  ameeleza namna ambavyo Dkt. Reginald Mengi alivyokisaidia Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati wakiwa kwenye hali ngumu ya uchumi kwenye kipindi cha uchaguzi.



“Mchango wake kwa CCM ni mkubwa sana, kuna kipindi tulipungukiwa fedha kwa ajili ya mawakala kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, tukaenda kwake akajaza fedha kwenye begi akasema ‘chukueni’.   Lakini hata hivyo mzee Mengi alikuwa habagui wanasiasa kwani aliwasaidia hata wale wa upinzani,” amesema Nape.

Ametolea mfano kuwa kwenye kuandika Ilani ya CCM alihusishwa kutoa mawazo kwenye sera za kiuchumi. Lakini Ukawa (umoja wa vyama vya Upinzani wakati wa Uchaguzi Mkuu 2015) walimhusisha sana katika Sera zao za kiuchumi na aliwasaidia kutoa mawazo.





Aidha, Nape ameleeza kwamba urafiki wake na Mzee Mengi haukuanzia katika siasa, Baba yake Nape (Marehemu Moses Nnauye) alikuwa rafiki Mkubwa wa Mengi na kwamba alikuwa mtu wa kipekee na pengine asingekuwa mfanyabiashara angeweza kuwa kiongozi wa Dini.



“Tumeangalia watu wenye ulemavu waliokuja hapa wengi wana baiskeli zinazofanana, mtoaji alikuwa ni Dkt. Mengi,” amesema Nape.



Nape ametoa Stori moja: Anasema ilikuwa sherehe za Mei Mosi mwaka fulani. Wakati viongozi na watu wengine mashuhuri wamekaa mbele, walishangaa kumuona Dr Reginald Mengi amesimama uwanjani na raia wa kawaida. Ilibidi wamuombe aondoke kule aje mbele kwenye jukwaa kuu. Nape anasema Mzee Mengi alianza kutembea peke yake kwa mwendo wake wa taratibu kuelekea mbele, akiwa peke yake, bila Mlinzi wala msaidizi.

Nape anaacha swali: Kwa ukubwa na fedha alizokuwa nazo Mzee Mengi, aliwezaje kujishusha kiasi hicho? (Sisi wengine, tukipata fedha kidogo tunajikweza na kujitenga na watu).





Kwa upande wake, Mwenyekiti a Chama Cha Demokrasia na Mandeleo (Chadema), Freeman Mbowe amesema asingeweza kubaki Dar es Salaam wakati wana ugeni mkubwa  Machame.



“Ilikuwa lazima tutangulie kuwekwa vitu sawa,” amesema Mbowe wakati akieleza sababu kwa nini hakuwepo katika shughuli za kumuaga Mzee Mengi pale Karimjee.



Pia amasema sababu nyingine ni kwamba yeye ni mtu wa karibu kabisa wa familia hivyo ilikuwa wajibu wake kuwahi huku kufanya shughuli za msiba na kwamba katika masuala ya kisiasa hawakuwa pamoja sana lakini licha ya kuwa na mwanachama wa chama kingine, hakutaka watu wabaguane kwa sababu ya itikadi za kisiasa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad