Ndege Ya Boing 737 Yashindwa Kutua Yatumbukia Mtoni

Ndege aina ya Boeing 737 imeshindwa kutua na kuishia kuingia mtoni nchini Marekani. Hiyo ni aina ile ile ya ndege iliyopata ajali na kusababisha vifo vya mamia ya watu nchini Ethiopia na Indonesia.



Kwa mujibu wa habari, ndege hiyo ilitoka katika barabara yake na kuingia mtoni wakati ikitaka kutua Florida nchini Marekani.



Tukio hilo limetokea katika uwanja wa ndege wa Jacksonville,ambapo ndege hiyo ya abiria iliyokuwa imebeba abiria 136 ilishindwa kutua na mwisho kuingia katika mto wa St.John. Hata hivyo hakuna aliyeripotiwa kupoteza maisha. Watu wawili wamejeruhiwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad