Muigizaji na mtangazaji Nick Cannon amejitokeza na kupinga taarifa zilizosambaa kuhusiana na yeye kutishiwa kuuawa baada ya kuapa kuiendeleza makala ya Dr. Sebi inayohusu kuwa kuna tiba ya dawa ya virusi vya UKIMWI pamoja na Saratani.
Ilielezwa kuwa makala hiyo ilikuwa ikiendelezwa na marehemu Nipsey Hussle ambaye alikua yupo tayari kuichapisha na kuiachia ili watu wapate kuifahamu. Mwimbaji huyo kupitia ukurasa wake wa instagram aliibuka na kukanusha stori hizo ambazo zilisema kuwa ameachana na makala hiyo baada ya kutishwa kuuawa na anaogopa kuishia kama Marehemu Nipsey Hussle.
“Oh wanatamani hii ingekuwa kweli, kwa aliyetengeneza hiki ni mjinga, siogopi” >>> aliandika Nick Cannon.
Inaaminika kuwa Rapper Nipsey aliuawa kutokana na harakati zake za kutaka kuiachia makala hiyo ambayo inaelezea kuwa kuna tiba ya dawa ya virusi vya UKIMWI pamoja na Saratani ambapo malalamiko mengi yalipelekwa katika serikali ya Marekani na kuihusisha kwenye mauaji hayo yaliotokea March 31,2019 mjini Los Angeles Marekani.
Nick Canon Aibuka na Kukanusha Taarifa za Kutishiwa Kuuawa Kisa Makala
0
May 31, 2019
Tags