Nyarandu Akamatwa na Polisi Kisa Hiki Hapa

ALIYEKUA Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM) na Waziri wa Zamani wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kabla ya kuhamia Chadema, amekamatwa na kuchukuliwa na watu wanaodaiwa kuwa wamekataa kujitambulisha akiwa kwenye kikao cha ndani cha CHADEMA kwenye Kata ya Itaja, wilaya ya Singida Vijijini mkoani Singida.



Nyalandu alikua kwenye zoezi la ‘Chadema ni msingi’ ambapo watu hao walifika wakiwa na silaha na kumchukua kwa nguvu na kutokomea nae kusikojulikana.



Wengine waliokamatwa ni Mwenyekiti wa kata hiyo na aliyekuwa mgombea ubunge wa Chadema wa jimbo hilo, David Jumbe.


Akizungumza na Global Tv Online, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, ACP Sweetbert Njewike amesema taarifa hizo ni za uzushi; “Ndugu mwandishi umefanya vyema kuniuliza, watu wanazusha uongo mitandaoni, watafuteni TAKUKURU watawapa ukweli wa jambo hilo, polisi hawajamkamata.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad