Ifuatayo ndiyo orodha ya maraisi kutoka nchi mbalimbali barani afrika waliofariki wakiwa bado wapo madarakani:
Lansana Conte, Rais wa GuineaBaada ya miaka 24 Lansana Conte alifariki na ugonjwa usiojulikana akiwa na umri wa miaka 74. Alipambana na matatizo ya kisukari na maradhi ya moyo. Kuanzia Aprili 1984 mpaka kifo chake Desemba 2008 alikuwa ni rais wa pili kushika madaraka nchini Guinea. Mbali na matatizo ya afya aliyokuwa nayo aliweza kushinda uchaguzi.
Omar Bongo, Rais wa GabonSaratani ya tumbo iliosambaa ndio iliyosababisha kifo cha Rais Omar Bongo June 2009 mjini Barcelona, Uhispania, baada ya kuwa rais kwa miaka 42 mfululizo. Alifariki akiwa na umri wa miaka 72 na pia alikuwa ni kiongozi aliyekaa madarakani kwa muda mrefu katika historia na alikuwa akiongoza katika mambo ya rushwa. Bongo alijikusanyia utajiri mkubwa huku akiiacha nchi yake katika hali ya umasikini.
Joao Bernardo Vieira, Rais wa Guinea-BissauJoao Bernardo Vieira rais wa Guinea-Bissau aliuwawa nchi mwake Machi 2009, akiwa na umri wa miaka 69. Alikuwa kiongozi wa nchi kwa muda wa miaka 31. 1978 alikuwa waziri mkuu na kuchukua madaraka 1980 na alitawala kwa miaka 19. Alibadilika na kuwa kiongozi wa umma na aliongoza miaka minne mingine zaidi. 2005 alishinda tena uchaguzi wa uraisi.
Umaru Musa Yar’Adua, Rais wa NigeriaUmaru Musa Yar’Adua, alifariki akiwa na umri wa miaka 58 mwaka 2011 akisumbuliwa na matatizo ya moyo nchini Nigeria. Alikuwa madarakani kwa miaka mitatu pekee. Alikosekana katika kampeni za uchaguzi kwa sababu za kiafya. Baada ya kuchaguliwa kwake 2007, afya yake ilidhoofika kwa haraka.
Muammar Gadhafi, kiongozi na mwana mapinduzi wa LibyaMwathirika wa mauaji, Muammar Gadhafi aliuawa akiwa na umri wa miaka 69 na vikosi vya waasi katika mazingira yasiyoeleweka nchini Libya, baada ya kuwa kiongozi wa taifa hilo kwa muda wa miaka 42. Aliuondoa uongozi wa kifalme bila ya kumwaga damu wakati wa mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 1969 lakini utawala wake ulifikia kikomo baada ya matokeo ya vuguvugu la mapinduzi ya uarabuni.
Malam Bacai Sanha, Rais wa Guinea-BissauKiongozi huyu alifariki mwaka 2012 alikuwa ni Malam Bacai Sanha rais wa Guinea-Bissau. Aliugua ugonjwa wa kisukari na alifariki mjini Paris baada ya miaka minne kama rais akiwa na umri wa miaka 64. Katika kipindi chote cha utawala wake alisumbuliwa na matatizo kadhaa ya kiafya yalosababisha kwenda hospitali mara nyingi.
Bingu wa Mutharika, Rais wa MalawiRais mwingine aliyefariki mwaka 2012 ni Bingu wa Mutharika, rais wa Malawi. Alipata mshutuko wa moyo mwezi Aprili na kufariki siku mbili baadae akiwa na umri wa miaka 78. Uongozi wake ulikuwa ni wa miaka nane na alipata mafanikio makubwa katika sera zake za kilimo na chakula. Sifa yake iliharibika kufuatia maandamano makubwa yalopinga ununuzi wa ndege ya rais iliyogharimu Dola milioni 14
John Atta Mills, Rais wa GhanaPia mwaka 2012, John Atta Mills, rais wa Ghana alifariki akiwa nyumbani kwake kwa mshutuko wa moyo na saratani ya koo akiwa na umri wa miaka 68. Alishinda uchaguzi wa rais wa 2008 alishika madaraka kwa miaka mitatu pekee. Alianzisha mikakati mingi ya kiuchumi na mageuzi ya kiuchumi yalomletea sifa kutoka ndani na nje ya nchi.
Meles Zenawi, Waziri Mkuu wa EthiopiaMeles Zenawi alifariki Agosti 2012 nchini Ubelgiji akiwa na umri wa miaka 57 kwa maambukizi yasiyojulikana. Ameiongoza Ethiopia kwa miaka 5 kama rais kuanzia mwaka 1991 hadi 1995 na kama Waziri Mkuu kwa miaka 17 kuanzia 1995 hadi 2012. Anajulikana kwa kuanzisha mfumo wa siasa wa vyama vingi, lakini pia kwa ukandamizaji wa maandamano halali ya watu wa Oromia wa kaskazini mwa Ethiopia.
Michael Sata, Rais wa ZambiaMichael Sata ni kiongozi wa hivi karibuni aliyefariki madarakani akiwa na umri wa miaka 77 kwa maradhi ambayo hayakuwekwa wazi Oktoba 28 2014, nchini Uingereza. Baada ya uchaguzi wa 2011, uvumi juu ya afya yake ulisambaa nchini Zambia. Kukosekana kwake katika shughuli kubwa za kitaifa kuliibua wasiwasi wa afya yake ingawa msemaji wake alisema alikuwa katika afya nzuri.