Pigania Ndoa Yako Si Michepuko ya Mumeo..



NIMEIKUTA MAHALI NIKAONA NI VIZURI KU-SHARE

Kuna dada mmoja nikikuwa namfahamu miaka mingi sana. Kama miama 15. Kipindi hicho tukiwa ni wasichana wa miaka 25. Dada huyo ghafla akawa na mahusiano na mume wa dada yangu. Nilimchukia sana. Dada yangu alimchukia sana. Wote tulimchukia. Alikuwa mlevi. Malaya na anayependa kuvaa uchi. Hakuwa anajijali hata kidogo.
Mimi na Dada yangu tulikuwa tunatamani hata afe ama akatike miguu kwa namna alivyokuwa malaya na mshenzi.

Miaka ikapita. Kila ninapokutana na dada yangu haishi kunikumbusha Dativa. Kila siku tulikuwa tunamuongelea. Na kutamani tusikie hata kuna msiba kwao na amefariki dunia.

Baada ya miaka mitano kupita. Mimi nikiwa nimeahamaliza masomo yangu. Na sasa na niko kazini nafanya kazi yangu nzuri tu. Kijana mmoja akaniambia ananipenda na anataka kunioa. Miaka yote hiyo sikuwa na mahusiano kwani nilijua na mimi kina Dativa wataharibu ndoa yangu. So sikupenda ndoa kabisa.
Hivyo kijana huyo nikamkataa. Ni kijana kama wa 10 hivi kumkataa.
Siku moja nikampigia dada yangu simu. Akanieleza mambo hayo kwamba hana raha na ndoa yake kwani anajua Dativa bado wana mahusiano na mumewe. Japo hawaoni ila anajua wanafanya siri. Dada yangu alikonda. Ni mwaka wa 7 sasa Dativa hajamtoka akilini.
Nilikuwa naumia pia.
Maisha yakasonga.

Nilipata safari ya mwenda mkoani Arusha.Jumapili Moja nikasema ngoja niende kanisani kuabudu Mungu. Ni kanisa la karibu tu lakini sio kanisa la imani yangu.
Siku hiyo nilipata msukumo hasa. Tena baada ya kujua muimbaji maarufu wa nyimbo za injili yuko hapo.Nilivaa vyema. Kisha nikajipeleka kanisani.
Ibada ilianza.
Ilikuwa nzuri sana.
Mh...Baada ya muda kidogo nikasikia mtangazaji akisema Familia ya Bwana na Bibi Juventus inataka kutoa shukrani.
Bwana Juventus na mkewe na watoto wao wawili. Wa kike mwenye 4 yrs na wa kiume mwenye 2 yrs.
Walisimama mbele.
Mwanaume alikuwa kavalia suti nzuri sana na kapendeza hasa. Mrefu. Bonge la handsome.
Watoto nao walipendeza sana. Walivalia vyema hasa.

Kisha huyo mwanamke alionekana mrembo. Aliyevalia nguo za thamani na kupendeza pia.
Nilimtazama sana mwanamke huyo. Ni kama niliyekuwa namfahamu. Nilijiuliza je ni mtangazaji ama nimemuona wapi?Sura yake ilinipotea kidogo. Pengine ni kwa namna alivuopendeza zaidi.
Nilipuuza. Ila ni familia iliyonivutia sana.
Kisha Mume akamshika mkewe bega na kumpa kipaza sauti na kumwambia ashukuru Mungu.
Mwanamke yule alianza kwakusema...

mimi na mume wangu na watoto wetu wapendwa. Tunazo kila sababu za kumahukuru Mungu kwa namna anavyitutunza na kutupigania kila mara. Na leo tuko mbele zenu kutoa shukrani zetu mbele ya Mungu na mbele ya kanisa kwa maombi yenu pia.
Mungu ametubariki na mwezi huu tarehe 10 tutasafiri kwa ajili ya huduma nje ya nchi. Maombi yenu ni ya Muhimu sana.

Mimi Dativa na Juventus tunawapenda sana. Mungu awabariki.
Moyo wangu ulifanya paaaaa... ulinipasuka paaaaaa...
Huyu ni Dativa?yule kahaba.. malaya... niliyekuwa natamani afe hata kesho?Leo ana ndoa na watoto na maisha mazuri?Nimebaki nakataa ndoa kwa sabau yake... kumbe yeye anasonga mbele?
Dada yangu naye analia kumbe Davuta ni wa viwango vingine?.Nilichukia... nikajikuta naumia zaidi na ninawaza kwamba Mungu hayuko fair.

Niliwaza mpaka watu wakanisikia. Mama mmoja akaniambia mbona unaongea mwenyewe?Nimasema kwanguvu..Mungu hayuko fair. Ana upendeleo.
Huyo mama akanimbia kwanini?
Nikamwambia Davita alikuwa malaya sana. Na kaitesa sana ndoa ya dada yangu.
Yule mama alinitazama na kutabasamu kisha akasema...
SIKIA MWANANGU... HUJUI KAMA MAKAHABA WATATUTANGULIA KWENYE UFALME WA MUNGU?

Mh.. akili ilinirudi.
Kisha nikatoka nje na kuiacha ibada ikiendelea. Na kumpigia dada yangu simu na kumwambia...
Dada nimemuona Davita. Ni mwanamke wa viwango vingime. Sio yule kahaba tena. Ni ana mume na watoto na ameokoka.
Hembu acha kumuwazia mabaya kabisa. Mungu amempendelea.

Kuanzia hapo nikajifunza jambo.
Hatupaswi kuwawazia watu mabaya wala kuwaombea mabaya.
Hembu na wewe nikusaidie leo.
Acha kuuwaza mchepuko wa mumeo. Waza maisha yako..songa mbele. Usisimame kuwaza mchepuko ambao saa yoyote utatubu dhambi mbele za Mungu na Mungu wetu ni Mungu wa Kusamehe. Badala yake kaza buti katika maisha yako Mungu akuinue.
......The End..........
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad