Rais Magufuli Awaombea Waislamu Ujenzi wa Chuo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametangaza kuwa Chuo Kikuu cha Kiislamu kitajengwa nchini kwa msaada wa serikali ya Saudi Arabia.

Ameyasema hayo kwenye kilele cha mashindano ya kusoma Quran tukufu, yaliyoandaliwa na taasisi ya Al-hikma na kufanyika katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam, ambapo Rais Magufuli alikuwa mgeni rasmi.

Rais Magufuli amesema, "minafahamu kuwa taasisi hii imekuwa ikifanya kazi kubwa, imejenga misikiti 50, imechimba visima 110, ina shule ya msingi moja na shule za sekondari mbili na katika hilo wanasomesha jumla ya yatima 400".

"Kwahiyo nilipokuwa nimekaa na sheikh Shariff (kiongozi wa taasisi ya Al-hikma) nilimchomekea na mimi mnijengee msikiti kule Chato na akakubali uwe msikiti wa 51 kwao. Na vilevile nilipoongea na waziri kutoka Saudi Arabia nikaona nimchomekee japokuwa hamkunituma, nilimtuma Waziri Mkuu afuatilie hawa ndugu zetu wanaweza kutusaidia kitu gani kikubwa hasa katika masuala ya elimu ya dini ya kiislamu, nikamuomba alisimamie vizuri hili suala la kuwa na Chuo Kikuu cha Kiislamu hapa Tanzania ambacho kitafadhiliwa na Saudi Arabia na amekubali", ameongeza Rais Magufuli.

Mashindano hayo ya Qur'aan ni ya 20 kufanyika nchini, ambapo mwaka huu yamehusisha jumla ya mataifa 18 barani Afrika na hatimaye mshindi aliyepatikana ni kijana Mouhamed Dialo wa Senegal aliyejishindia kiasi cha Sh 20 milioni za Kitanzania.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad