Rais Magufuli amesema Serikali imeyachukua mapendekezo yote na ushauri wa TUCTA likiwemo la kuangalia namna ya kupunguza suala la kodi ya mfanyakazi kuwa ya tarakimu moja.
Pia bodi za misharaka kukutana na kujadiliana kuhusu viwango vya mishahara ya wafanyakazi.
"Kuhusu suala la kupunguza kodi halina tatizo, kama tumeweza kupunguza kodi kutoka asilimia 11 hadi tisa bado tunaweza kuendelea kujadiliana," amesema Magufuli.
Awali TUCTA ilieleza kuwa, punguzo la kodi katika mishahara kutoka 11% hadi 9%, linawanufaisha wafanyakazi wenye mishahara kati ya 170,000 hadi 325,000 pekee. Wenye mishahara zaidi, hawanufaiki. Wameiomba serikali, punguzo hilo la hadi 9% liwe kwa wafanyakazi wote.