RAIS Magufuli Kushangiliwa kwa Nguvu Afrika Kusini Ina Maana Gani kwa Wapinzani wake??
0
May 26, 2019
Marais wengi wameenda kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa Afrika Kusini 25 May 2019 , lakini mara baada ya jina la Rais wa Tanzania John Magufuli kutajwa kwamba anaingia uwanjani ,Raia wa Afrika kusini walisimama na kushangilia kwa nguvu sana.
Umati mkubwa wa wananchi umelipuka kwa shangwe na chereko wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipowasili katika uwanja wa michezo wa Loftus Versfeld jijini Pretoria kuhudhuria sherehe za kuaishwa kwa Rais wa Afrika ya Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa leo Jumamosi Mei 25, 2019
Kwa Mtazamo Wa kawaida hii inaashiria Rais Magufuli Kukubalika KITAIFA NA KIMATAIFA,
Kwa upande wa upinzani Utaendelea Kubeza na kukejeli Hatua Ambazo anafanya Rais Magufuli ila Kwa upande Wangu wapinzani Kufanya hivyo ni Sahihi kwao kwasababu Hauwezi Kutafuta Serikali kwa kusifia Serikali Iliyopo.
Wananchi Wanatakiwa kufahamu Wapinzani wanatekeleza Majukumu Yao,ila Ukweli wanaufahamu na Ukweli siku zote Haufichiki.
Kwa Wapinzani Kwasababu ya Kupinga hata yale Mazuri yanayofanywa Na Rais Hawachelewi Kusema .
"Waliomshangilia Rais Magufuli Afrika kusini Ni wanaCCM Walisombwa na Magari"
Ndugu Kwa sasa Hatuhitaji Kukosoa kila Kitu Tunahitaji kusema pale Panapohitaji Kusema,
Tuna Vijana wengi Ambao wana uwezo Mkubwa wa kulisemea Taifa hili na Sio Kushambulia Viongozi kwa Matusi Mitandano.
Tags