Rais Museni ataka nchi za Afrika kuondoa ukomo wa kuwania urais

Mwezi mmoja baada ya Mahakama ya Juu nchini Uganda kuunga mkono hatua ya bunge kuondoa ukomo wa kuwania urais nchini humo, Rais wa nchini Yoweri Museveni anataka mataifa ya Afrika yaondokane na sheria zinazowazuia viongozi wenye umri mkubwa kuwania urais katika nchi zao.

Rais Yoweri Museveni wa Uganda anataka nchi za Afrika kukubali kubadlisha katiba zao kuondoa vizuizi  vinavyowakataza viongozi wenye umri mkubwa na wale ambao wametawala kwa muda mrefu kuwania urais.

Rais Yoweri Museveni amesema kwamba ukomo uliowekwa kwenye katiba kama vile ukomo kwa mihula na ukomo kwenye umri vinazuia Afrika kuwa na viongozi wazuri na wenye uzoefu.

Rais Museveni anajiandaa kugombea tena katika uchaguzi wa urais mwaka 2021 na akishinda, atakuwa mmoja wa viongozi wa Afrika waliotawala muda mrefu zaidi (miaka 40).

Bunge la Uganda limebadilisha katiba mara mbili na kumpa nafasi Museveni kuwania kwenye kiti cha urais. Mnamo mwaka 2005, bunge liliondoa ukomo wa mihula na mwaka 2017 likaondoa ukomo wa umri wa miaka 75 nakumpa nafasi Museveni kuwania kwenye kiti cha urais mwaka 2021.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad