Rais wa Liberia na nyota wa zamani wa soka George Weah, amerejea tena kazini , wiki mbili kamili baada ya kuitoroka ofisi yake kwasababu nyoka wawili walikuwa wamepatikana katika jengo la ofisi yake.
Jengo hilo lilitakiwa kusafishwa vizuri kwa kemikali ya kuua nyoka kabla rais kushauriwa kurejea ofisini kwake Jumatano.
Mmoja wa watu wa kwanza kumtembelea rais Weah katika ofisi yake alikuwa ni Makamu rais wa zamani Joseph Boakai, aliyeshindwa na Weah katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2017.
Bwana Weah alizungumzia juu ya juhudi za serikali yake za ''kulinda misingi ya demokrasia'', na kuwavutia wawekezaji wa kigeni iki kuinua uchumi, taarifa hiyo ilitumwa kwenye wavuti wa serikali.
Rais amekuwa akifanyia kazi katika ofisi iliyopo ghorofa ya sita ya jengo la Wizara ya mambo ya nje tangu jengo jirani na ofisi ya rais lilipoungua kwa moto mwaka 2006.
Nyoka wawili weusi ambao walitoka kwenye shimo lilolokuwa kwenye sehemu ya mapokezi ya jengo la ghorofa sita walikwenda nyuma ya jengo hilo ghafla wakati watu walipokuwa wakijaribu kuwauwa.
Baada ya tukio hilo maafisa wa polisi na maafisa wa usalama wa rais walionekana wakiyalinda makao ya Bwana Weah katika mji mkuu wa Monrovia.
Nyoka wamfurusha rais wa Liberia kutoka afisini mwake
Weah atoa sheria ya 'kibaguzi' ya uraia
Wenger apatwa na mtego wa habari za uzushi
Kanda ya video iliochapishwa katika ukurasa wa kwanza wa gazeti la African News ilionyesha wafanyikazi wakijaribu kushambulia nyoka wakati walipoonekana katika eneo la kukaribisha wageni la jengo hilo.
Jumba hilo limekuwa katika eneo hilo kwa miaka kadhaa sasa kwasababu yamfumo wa maji taka , na maafisa wanasema kuna uwezekano wa nyoka kuingia katika jumba hilo.
Haijafahamiika ikiwa nyoka hao waliuawa au la.
Rais wa Liberia Arejea Ofisini Baada ya kuingiliwa na nyoka
0
May 02, 2019
Tags