Kutokana na kauli zilizohusisha kabila la Wachaga (kwamba ni ajabu Mchaga kutoa fedha kwa walemavu) zilizotolewa na Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam wakati wa kumuaga Dkt. Reginald Mengi katka ukumbi wa Karimjee, Katibu Mku wa CCM Dkt. Bashiru alisema anaomba msamaha kwa niaba ya RC Makonda.
Baada ya hapo, Mkuu wa KKKT, Askofu Shoo aliwaita Rc Makonda na Freeman Mbowe akisema hiyo ni ishara ya kusameheana na mariadhiano na kuwataka wapeane mikono.
Baada ya kupeana mikono RC Makonda alizungumza na kusema hakuwa na nia mbaya ila tafsiri imeleta shida hivyo anaomb radhi 'kutokana na tafsiri'.
“Nashukuru sana kwa maelekezo na maonyo ya Baba askofu, Lakini la pili nashukuru sana kwa katibu wangu Mkuu wa chama cha mapinduzi kwa kusimama na kuomba radhi kwa niaba yangu huu ni upendo wa hali ya juu sana," ameeleza.
Ameendelea kwa kusema,"Lakini la tatu namshukuru sana kaka yangu Freeman Mbowe ambaye mimi na yeye tunafahamiana kwa muda mrefu sana na mbele ya rafiki yetu kipenzi Baba yetu Reginard Mengi kuyatamka yale ambayo yalimkwaza nae nampa shukrani sana angeweza kukaa kimya”.