Waandamanaji wapatao sita na mtu mmoja wa kikosi cha usalama wameuwawa katika mapigano yaliyotokea katika mji mkuu wa Sudan , Khartoum.
Watu hao waliuwawa kwa risasi wakiwa nje ya makao makuu ya jeshi na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati ambapo raia walikuwa wanaandamana kudai serikali kuongozwa na raia.
Waandamanaji wanasema askari walikuwa wanahusika na tukio hilo ingawa askari wenyewe wanakana kuhusika na tukio hilo na kuwalaumu watu wasiojulikana.
Ramadhan 'inavyoimarisha' maandamano Sudan
Bashir ashtakiwa kwa vifo vya waandamanaji
Sudan imekuwwa katika serikali ya mpito tangu mwezi uliopita mara baada ya rais Omar al- Bashir kuondolewa madarakani.
Waandamanaji wamekuwa wakiandamana kuzunguka makao makuu ya jeshi tangu tarehe 6 mwezi Aprili , siku tano mara baada ya jeshi kumpindua Omar al-Bashir ambaye alitawala Sudan kwa miaka 30.