Sakata la DECI: Bil.14.3, Nyumba na Magari Vyataifishwa

Sakata la DECI: Bil.14.3, nyumba na magari vyataifishwa
Mahakama Kuu Tanzania, imeamuru mali zote zinazomilikiwa na Kampuni ya Development Enterpreneuship for Community Initiative (DECI) yakiwemo magari, nyumba na Sh.Bilioni 14.3 kutaifishwa kuwa mali ya Serikali.

Pia, imemwagiza Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kubadilisha umiliki wa magari kutoka DECI kwenda kuwa ya serikali na imemuagiza Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) kuwasilisha maombi mahakamani ili madalali wakawahamishe wananchi wanaoishi kwenye nyumba hizo kuwa za serikali.

Hukumu hiyo imesomwa na Jaji Stephen Magoiga ambapo amesema mali zisizohamishika ikiwamo nyumba zibadilishwe majina ya umiliki kutoka DECI kuwa kwa jina la Msajili Hazina.

Kuhusu akaunti za kampuni hiyo zenye Sh. Bilioni 14.3 Jaji amesema zihamishwe kutoka kwenye matawi yao kwenda Serikalini mara watakapopokea amri ya mahakama yake.

Uamuzi huo unatokana na maombi ya msingi ya DPP ambapo aliwasilisha maombi hayo mahakamani hapo, akiiomba itoe amri ya kutaifishwa kwa mali za kampuni hiyo yakiwamo magari 11, nyumba na viwanja vinane na fedha ziwe Mali ya Serikali.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad