Sakata la Urusi kuingilia uchaguzi Marekani lashika sura mpya, Mwanasheria Mkuu agoma kuhudhuria kikao cha bunge

Waziri wa Sheria wa Marekani William Barr amewafahamisha wajumbe wa kamati ya sheria ya bunge la Marekani kwamba hatohudhuria kikao kuhusu ripoti ya mchunguzi maalumu Robert Mueller, hali inayozidisha mvutano kati ya wabunge wa chama cha Demcrats na wizara ya sheria.


Kwa mujibu wa shirika la habari nchini Ujerumani la Deutsche Welle, Uamuzi wa Barr uliotakana na tofauti kuhusu maswali alioulizwa na kamati hiyo, umetokea wakati ambapo wizara yake imeshindwa kutekeleza agizo la kuwasilisha ripoti kamili ya uchunguzi wa Mueller kuhusu madai ya uingiliaji wa Urusi katika uchaguzi pamoja na ushahidi wake.

Hatua hizo zinaweza kusabaisha kura ya kumuwajibisha Barr kwa kudharau bunge, na yumkini kutolewa hati za kuitwa mahakamani jambo linaloweza kusababisha mapambano ya muda mrefu mahakamani kati ya Wademocrat na utawala wa rais Donald Trump.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na wizara ya sheria, mwenyekiti wa kamati ya bunge inayoshughulikia masuala ya sheria, Jerrold Nadler aliweka masharti mapya kabisa na yasiyokuwa ya lazima kwa waziri Barr.

Hata hivyo, mwenyekiti huyo wa kamati ya sheria amesema ataendelea na kikao cha leo, na kuweka uwezekano wa kuwa na kiti kitupu cha shahidi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad