Samatta Atwaa Tuzo ya Mchezaji Bora Ubelgiji

Nahodha wa Taifa Stars, anayecheza katika Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa tatu wa Genk kutwaa tuzo hiyo iitwayo Ebony Shoe Award.

Mchezaji wa kwanza wa KRC Genk kutwaa tuzo hiyo ni Souleymane Oulare raia wa Guinea aliyeshinda mwaka 1999 na wa pili ni Moumouni Dagano raia wa Burkina Faso aliyeshinda tuzo hiyo mwaka 2002.

Tuzo inayomaanisha kuwa kwa sasa Samatta ndiye mchezaji bora mwenye asili ya Afrika anayesakata soka Ubelgiji.

Ubora wake unathibitishwa na magoli 23 aliyofunga hadi sasa kwenye ligi akiwa ndio kinara.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad