Serikali Kuajiri Watumishi Wapya 44,800 kwa Kipindi cha 2019/20

Serikali Kuajiri Watumishi Wapya 44,800 kwa kipindi cha 2019/20
Watumishi 44,800 wataajiriwa katika taasisi za Serikali kwa kipindi cha 2019/20

Hayo yameelezwa na naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Dk Mary Mwanjelwa jana Jumanne Mei 28, 2019. na kubainisha kuwa ajira hizo zitawalenga Watanzania wenye sifa.

Dk Mwanjelwa alisema kuwa si Serikali pekee ndio inayotakiwa kutoa ajira, hata watu binafsi wanaweza kutoa ajira kwa vijana.

Naibu Waziri huyo alikuwa akijibu swali la mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Aida Khenan aliyehoji kama kuna utaratibu wowote wa kuajiri watu waliohitimu vyuo na kukidhi vigezo vya kuajiriwa.

Katika swali la nyongeza mbunge huyo amehoji kwa nini Serikali inaendelea kuweka vigezo vya uzoefu kazini wakati inajua hakuna vijana wenye uzoefu.

Katika majibu yake, Dk Mwanjelwa alisema duniani kote Serikali si mwajiri pekee, akitolea mfano waajiri wengine ambao ni sekta binafsi, mashirika, asasi za kiraia na maeneo mengine.

Kuhusu uzoefu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenister Mhagama alisema wameondoa uzoefu badala yake Serikali imeanzisha kozi maalum kwa wahitimu ambazo husaidia kuwapa ujuzi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad