Serikali Kuendelea Kuchukua Hatua Dhidi Ya Wamiliki Wa Kumbi Za Starehe Wanaopiga Muziki Mnene Na Kuwa Kero Katika Makazi Ya Watu.

Serikali imesema itaendelea kuwachukulia hatua kali za kisheria  wamiliki wa  Bar kote nchini  wanaopiga muziki mkubwa katika bar zilizokaribu na  Makazi ya watu na kusababisha kero kwa Wakazi husika na kukosa usingizi.

Rai hiyo imetolewa leo Mei 22,2019 na Waziri wa Ofisi ya Rais[TAMISIMI]Mhe Seleman Jafo wakati akijibu swali la mbunge wa  Viti Maalum Maryam Salum Msabaha aliyehoji ,kuna baadhi ya Bar na Club ambazo zimejengwa kwenye makazi ya watu  ambazo zimekuwa na kero kwa jamii kwa kupiga muziki mkubwa na usiozingatia  Maadili ya Kitanzania, je,nini kauli ya Serikali kuhusu Bar  na Club  ambazo zinakiuka  maadili ya jamii na sheria.

Katika majibu yake ,Waziri wa Ofisi ya Rais ,TAMISEMI Mhe.Seleman Jafo amesema serikali inawaelekeza wamiliki wote wa Bar na Club kuzingatia maelekezo ya  sheria ya Vileo  Na.28 ya Mwaka 1968  kifungu cha 14[1] katika uendeshaji wa shughuli zao  ambapo amesema serikali haitasita kuchukua hatua  kwa vitendo vyovyote  vitakavyobainika kukiuka sheria na kusababisha kero kwa wananchi wengine.

Kutokana na Bar na Club  kuwa  kero katika makazi ya Watu kwa kupiga muziki mkubwa ,Waziri Jafo amewaagiza viongozi wa Serikali za mitaa wakiwemo wakuu wa wilaya na Mikoa  kote nchini kufuatilia jambo hilo .

Naye Mbunge wa Rombo,Joseph Selasini amehoji,Mara nyingi Bar zimekuwa zikijengwa kwa kutozingatia mipango miji  na watu wenye Madaraka wakiwemo wabunge wenyewe  kwanini Serikali isitoe tamko juu ya Bar zinazojengwa Ovyo ovyo iwe Marufuku na mtu atakayetoa kibali cha ujenzi akamatwe.

Akijibu swali hilo,Waziri Seleman Jafo amesema sheria zipo na kinachotakiwa ni kusimamia sheria husika kwa viongozi wa serikali za mitaa na kufanya ufuatiliaji dhidi ya wamiliki wa Kumbi za starehe wanaokiuka sheria hizo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad