Polisi nchini Uganda inamshikilia tangu Jumatatu wiki hii mwanamuziki na mbunge wa Kyadondo, Robert Kagulani a.k.a Bobi Wine na tayari amefunguliwa mashtaka.
Bob Wine alipandishwa kizimbani katika mahakama moja jijini Kampala na kusomewa mashtaka ya kuandaa mkutano na kufanya maandamano kinyume cha sheria mwaka 2018 na baadaye kuzuiwa katika Gereza la Luzira.
Mmoja wa wanasheria wa Bob Wine, Asuman Basalirwa amesema mteja wake amekamatwa kwa sababu za kisiasa. Msanii huyo anatajwa kuwa tishio kwa mustakabali wa siasa za rais Yoweri Kaguta Museveni.
Hata hivyo Serikali kupitia kwa naibu msemaji, Shaaban Bantaliza, anasema Bob Wine pamoja na watu wengine wanaopenda kuandamana bila kufuata sheria hawataachwa na mkono wa sheria.
Serikali ya Uganda Yasema Bob Wine Anapenda kuandamana biyla Kufuata Sheria
0
May 01, 2019
Tags