Serikali Yafuta Mkataba wa Kununua Korosho

Serikali imeufuta mkataba huo uliowahi kutajwa kuwa na thamani ya Shilingi za Kitanzania Bilioni 400. Tarehe 30 Januari mwaka huu Serikali iliweka wazi kuwa imeingia mkataba na Kampuni ya kutoka nchini Kenya ya Indo Power Solutions Ltd iliyojinasibu kuwa na uwezo wa kununua Korosho tani 100,000.



Serikali kupitia Waziri wa Biashara, Joseph Kakunda imesema kampuni hiyo imeshindwa kutekeleza sehemu ya makubaliano hivyo mkataba umekufa.



Aidha, Februari 01, 2019 JamiiForums iliibua madudu ya kampuni hiyo na kuyaanika wazi(Link kwenye bio) kitendo kilichozidi kuianika kampuni hiyo ambayo ilionekana wazi ni kampuni isiyo na uwezo uliokuwa ukinadiwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad