Serikali yagoma ongezeko la mshahara kwa Walimu 'sio deni'

Serikali imesema nyongeza ya Walimu ya mshahara haipaswi kuombwa au kudaiwa bali serikali ndio inauamuzi wa kutoa ua kutotoa.

Kauli hiyo imetolewa leo bungeni na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi), Mwita Waitara wakati akijibu swali kwa niaba ya waziri wa utumishi, menejimenti ya umma na utawala bora.

"Nyongeza ya mwaka ya mshahara haipaswi kuombwa au kudaiwa na waalimu bali serikali ndio ina uamuzi wa kutoa au kutotoa nyongeza hiyo kutokana na sera za kibajeti kwa mwaka husika," amesema Waitara.

Kulingana na kanuni za kiutumishi ambazo watumishi wote wanajua, Kwa mfano kwa mwaka wa fedha 2019/20 kama hatukuingiza kipengele cha nyongeza ya mshahara ambalo mnajua kuna tamko limetolewa Mei Mosi maana yake ni kwamba mwaka huu kama wataongezwa mishahara halipaswi kuwa deni kwa kanuni za Kiutumishi Watumishi wote wanajua," ameongeza Waitara.

Aidha Waitara amesema Serikali itaendelea kutoa nyongeza ya mwaka ya mshahara kwa watumishi wote kadri uwezo wa kulipa utakavyoruhusu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad