Serikali imebainisha kuwa imekwisha ipatia Kampuni ya Azam Media Ltd leseni ya kurusha matangazo kwa chaneli za bila malipo na kwamba kampuni hiyo imeahidi kufunga mitambo yake nchi nzima kwa ajili ya kurusha matangazo hayo ndani kwa kipindi cha miezi saba.
Hayo yameelezwa leo Bungeni na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditiye ambaye ameeleza kuwa Azam Media Ltd jana wamepokea leseni ya kuonyesha chaneli za ndani bure.
Nditiye amesema katika kipindi cha miezi saba watajenga mfumo wa kurusha chaneli hizo, hivyo wananchi wanapaswa kuvuta subira wakti hilo likifanyiwa kazi.