Serikali Yamezidi Kutoa Tahadhari Kuwepo Kwa Ugonjwa wa Homa ya Dengue


Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imezidi kutoa tahadhari ya  kuwepo kwa ugonjwa wa homa ya Dengue nchini hususani katika Jiji la Dar Es Salaam na Tanga.

Tahadhari hiyo imetolewa leo na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Kambi wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za wizara hiyo zilizoko jijini Dodoma.

Prof. kambi amesema hadi kufikia 6 Mei 2019, kati ya watu waliopimwa, wagonjwa 1237 wamethibitishwa kuwa na virusi au walikwishapata ugonjwa wa Dengue na kati yao 1150 ni kutoka Dar Es Salaam, 86 ni kutoka Tanga na mtu mmoja kutoka Singida.

Aidha, Prof Kambi amesema takwimu za ugonjwa wa Dengue kwa kipindi cha Januari hadi Aprili 2019 zinaonesha mwenendo wa ugonjwa huu kuwa na idadi ya wagonjwa 1237, vifo vya watu wawili na kuongeza kuwa waliofariki walikua na maradhi mengine.

Pamoja na hayo Mganga Mkuu huyo wa Serikali amelipongeza jiji la Dar Es Salaam kwa kuanza kunyunyizia dawa viuadudu (Biolarvicides) kwa ajili ya kuangamiza mazalia ya mbu ili kupambana na ugonjwa huu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad