Shahidi ajichanganya kwenye kesi ya mauaji ya mwanafunzi

Mtuhumiwa namba moja wa kesi ya mauaji Hamis Chacha ambaye ni mlinzi wa Shule ya Scolastica ametoa ushahidi wake kuhusiana na mashitaka yake ya kutuhumiwa kumuua mwanafunzi wa shule hiyo Humphrey Makundi, Hamis Chacha ameto ushahidi wake na kukiri kuwa 15 November 2017 walichukua maelekezo yake bila ya yeye kupigwa.
Chacha ambaye ni shahidi wa kwanza na mtuhumiwa pia katika upande wa utetezi amesema polisi walifika katika shule hiyo ambapo ndio mahali linapodaiwa kutokea tukio la mauaji ya mwanafunzi wa shule hiyo Humphrey Makundi, Makundi alikuwa akisoma katika shule ya Scolastica aliuwawa usiku wa November 6 2017 na mwili wake kutupwa mto Ghona ulio umbali wa mita 300 kutoka shuleni hapo.
Akiongozwa na wakili Kipoko amedai kwamba zana za kazi alizokabidhiwa shuleni hapo ni magwanda pamoja na panga ambalo alikuwa akilitumia katika shughuli zake za ulinzi, Shahidi huyo amesema 18 November 2017 aliongozana na askari aliokuwa nao nakupatikana kwa panga linalodaiwa kutumika katika mauaji hayo.
Mtuhumiwa huyo wakati akiulizwa maswali na wakili wa upande wa mashtaka Abdala Chavula anadaiwa kutoa maelezo yanayotofautiana ambapo  12 April 2019 kesi ikiendelea aliiambia Mahakama alipelekwa kwa ulinzi wa amani kwa ajili ya ungamo la kukiri kuhusika na mauaji hayo
Kesi hiyo namba 28 inawakabili watuhumiwa watatu akiwemo Hamis chacha mlinzi wa shule hiyo, Edward Shayo mmiliki wa shule hiyo pamoja na Laban Nabiswa mwalimu wa taaluma katika shule hiyo. Kesi hiyo imeahirishwa hadi May 7 2019 ambapo mshtakiwa wa kwanza anayetuhumiwa na mauaji ya mwanafunzi huyo ataendelea na utetezi wake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad